IPI DINI YA KWELI NA UZIMA Tunapozungumzia mada hii ya DINI inatupasa kuelewa kwamba hii ndio njia yetu ya kutufikisha kwa MUNGU. Marafiki zetu wakiislamu wanadai kwamba uislamu ndio DINI ya haki. Sasa tuangalie kwa maandiko kama jambo hilo ni la kweli. Kwanza kabisa ni vyema tuelewe tunapozungumzia swala hili tuna maanisha nini. ‘’DINI’’ maana yake ni nini? Unaposoma Quran 3:99 inatuonyesha kwamba neno hili DINI linamaanisha NJIA. Pia unaposoma Biblia Ayubu 4:6 inasema Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako? kwa hivyo tunapata kwamba maana ya neno dini ni njia. Kwa hivyo ni ipi njia ama dini ya kutufikisha kwa MUNGU. waislamu wanasoma andiko hili na kutaka kuonyesha kwamba uislamu umekuwapo tangu Adam hadi leo. Andiko wanalolisoma ni hili. Quran 2:213…”watu wote walikuwa Dini moja ya haki aliyokuja nayo nabii Adam kisha wakahitalifiana kwayo…’’[tafsiri ya Al farsey] Lakini ukisoma tafsiri zingine kama vile Al Muhsin Al Barwani utapata kwamba ametafsiri kama ilivyo katika lugha ya kiarabu ikasema ‘’watu wote walikuwa ummah mmoja’’ kwa hivyo unapata kwamba neno dini hapo halipo. Kisha wanasoma pia Qurani 30:30…kwamba umbile la mwanadamu ni uislamu. Sasa hapo pia wanaweka sana mkazo wakusema kwamba kumbe umbile la mwanadamu ni uislamu. Lakini sasa hebu tuingie kwenye maandiko ili tuweze kuelewa jambo hili. Ukisoma Quran 42:13…’’Amekupeni sharia ya dini ile ile aliyomuhusia Nuhu na tuliyo tuliyokufunulia wewe na tuliyowausia Ibrahimu na Musa na Isa…’’ lakini ukiangalia hapa hapajatajwa ni dini ipi andiko limesema tu dini ile ile. Sasa swali linakuja hapa ni hili, ni dini ipi hii ambayo Muhammad alifunuliwa tu ? na ukumbuke yeye Muhammad hakuusiwa hio dini bali alifunuliwa tu. Tunasoma Quran 2:62…katika walioamini mitumw ya zamani huko na Mayahudi na Wakristo na wasabai(maneno hayo yanayofuata katika aya hio sasa kama anavyosema Muhammad hayapatikani katika nakala ya kiarabu kwa hivyo hayana msingi wowote) kwa hivyo tunapata kwamba dini iliyotangulia ambayo Muhammad ameonyeshwa tu ni wakristo ambao walitangulia. Na hili msomaji liko dhahiri kabisa katika qurani kwa kudhibitisha Zaidi tazama katika quran tafsiri ya Al Barwani 4:131 katika ufafanuzi wa aya hiyo anasema…’’tumewausia watu wa dini zilizotangulia toka mbinguni, katika watu wa kitabu..’’ na anazidi kusema kwamba, ‘hapana kitu kilichotoka nje ya utawala wake.’ Sasa swali linguine ni hili, watu wakitabu ni kina nani? Tunasoma hiohio tafsiri ya Barwani 16:125 ufafanuzi wa hio aya inasema hivyi, ‘na jadiliana na watu na watu wa dini zilizotangulia katika watu wa Biblia yaani mayahudi na wakristo’ kahivyo ni wazi kwamba wakristo wamekuwapo tangu zamani kuliko waislamu. Swali lingine linajitokeza hapa, Je! Manabii walikuwa wa dini ipi? 1 Petro 1:10… Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. 11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo Kumbe sasa tunaona ya kwamba manabii wote walikuwa ni wakristo kwa sababu Roho wa Kristo alikuwa ndani yao. Jiulize hivi, ROHO wa KRISTO akiwa ndani yako ama wewe ukiwa ni mfuasi wa KRISTO utaitwa vipi? Tumuulize YESU KRISTO mwenyewe atuambie. Marko 9:41 inasema hivi… Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake. Sasa tuchunguze manabii wa zamani mmoja baada ya mwingine ili tubainishe ukweli wao. Tuanze na Ibrahimu. Wagalatia 3:29… Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi. Kwa hivyo bila kupinga tunapata kuwa Ibrahimu hakuwa muislamu bali alikuwa mkristo. Je! YESU Anadhibitisha hayo? Tusome Yohana 8:58… Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Kumbe Biblia inadhibitisha jambo hilo kuhusu Ibrahimu kuwa mkristo. Tumuangalie pia Musa naye alikuwa wa dini gani? Tusome Matendo 7:37… Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye. 38 Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi. Swali la kujiuliza ni kwamba, wanaoingia kanisani ni akina nani? Bila shaka ni wakristo. Na kama unaingia kanisani wewe unakuwa mkristo. Sasa swali linakuja hivi, Imani hii yetu kama wakristo inatoka wapi ama ilianza na nani? Tusome Waebrania 12:2…tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. Kumbe Imani hii yetu ilianzishwa na YESU KRISTO mwenyewe. Na kama Yeye ndiye kaianzisha ilikuwa lini na wapi? Yohana 17:5…na sasa Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. Kumbe Imani hii yetu ilikuwepo hata kabla ya ulimwengu kuwako na ndio sababu Yeremia akiongozwa na ROHO MTAKATIFU alisema hivi, Yeremia 6:16… Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo. Kumbe Mungu Anatusihi turudi katika njia hio ambayo niya salama. Na hii ndio sababu marafiki zetu waislamu wanaambiwa waitafute njia ya kufikilia pepo ya Mwenyezi MUNGU. Hio ni katika Qurani 5:35. Kwanini wanaambiwa waitafute njia, ni kwa sababu hawana njia ndio maana kila siku katika swala zao mara tano kwa siku wanaomba hivi, Qurani 1:6… tuongoze katika njia iliyonyoka…hii ni kwa sababu hawajaipata hio njia. Sasa kwa sababu hawana njia, sisi ambao tuna hio njia tunapaswa kufanya nini? Mathayo 7:7…Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; 8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Sasa kwa kuwa wamebisha kwetu wakristo ambao tuna hio njia sasa tuwape hio njia tena kwa upendo mwingi. Hio njia ni ipi? Yohana 14:6…Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kumbe NJIA yetu ni YESU KRISTO na kwa hio NJIA peke yake ndio itakayo kufikisha kwa BABA. Kama sasa tumepata njia ya uzima hizi njia zingine zitakuwa vipi? Mithali 16:25… Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti. Kwa hio njia zingine kama si ya YESU KRISTO hio njia huenda ni ya mauti naukitaka salama njoo kwa YESU KRISTO. Lakini ukirudi nyuma kidogo, waislamu wanadai eti kwamba uislamu ni umbile la mwanadamu na wanasoma Qurani 30:30…’’ndilo umbile alilowaumbia wanadamu’’ kwa hivyo wanadai kwamba kila mwanadamu anzaliwa akiwa muislamu. Lakini tujiulize swali moja, ikiwa uislamu umekuwapo tangu zamani inakuwaje kwamba Muhammad anaamrishwa kuwa wa kwanza kusilimu? Soma Qurani 6:14. Ukisoma Qurani 6:122 utapata maana kamili ya kusilimu. Kumbe Muhammad ndiye wakwanza wa kusilimu na hio haiwezi kuwa uislamu ulikuwapo tangu zamani. Pia soma Qurani 12:19-20 tafsiri yake hapo chini inasema hivi…unaona, kuuzana kulikuweko miaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliokuja nayo nabii Muhammad…kumbe ni wazi uislamu umeanzishwa na Muhammad. Ushahidi huu hapa, Qurani 10:104…enyi watu, ikiwa munayo shaka katika dini yangu. Kwa hivyo hio dini niya Muhammad. Kwa hivyo tunapata kuwa Muhammad yeye kaianzisha hii dini kasha akaanza kumpambia MUNGU na kumpa hio dini ambayo MUNGU haijui kabisa. Ndio sababu alianza kuwaambia hivi, Qurani 3:19 ikasema ‘’Bila shaka Dini ya haki mbele ya mwenyezi Mungu ni uislamu’’.kama hio dini ni Mungu angalisema kwamba hio dini ni yake. Lakini hatupati hilo kamwe. Na kwa sababu hio vitisho vilianza kwakusema hivi Qurani 3:85…’’na anayetaka dini isiyo ya kiislamu basi haitakubaliwa kwake’’ sasa hivi ni vitisho tu na hili linatuonyesha kuwa hii dini ya kiislamu haijaja ili kuelekeza watu kwa Mungu. Ukisoma Qurani 42:10 inatupa kibali cha kuingia katika vitabu vingine kando ya Qurani yaani hadithi. Ukisoma hadithi inaitwa Alu’lu walmarjani hadithi ya 14 ukrasa wa 9 inasema hivi, Imepokewa na Abu Huraira[r.a] kuwa, mtume wa Allah[s.a.w] amesema ,’’nimeamrishwa niwapige vita watu mpaka waseme, ‘Hakuna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah’, kwa hivyo hii inatuonyesha wazi kuwa hii dini niya kulazimisha watu. Pia ukisoma kitabu kiitwacho Maisha ya nabii Muhammad ukrasa wa 18 kinasema kwamba muislamu wa mwanzo kabisa duniani ni mwanamke jina lake ni bi Khadija mkewe Muhammad. Sasa rafiki yangu, ina maana gani kumfuata ambaye hajui atakapokupeleka? Ni heri uwe katika mikono ambayo itakujali na hata kukufikisha kwenye ufalme wa MUNGU. Muhammad ametueleza yeye hajui atakavyo fanywa wala wanaomfuata Qurani 46:9 lakini YESU KRISTO Anajua atakapotupeleka. Soma Yohana 14:1… Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Ni vizuri ndugu na dada mpendwa kufuata njia ile ambayo itakufikisha kwa Mungu na hio njia ni YESU KRISTO. JAMBO LINGINE ni kwamba, hii dini ya uislamu imeletwa duniani ili kushinda dini zingine wala haina uzima ukiifuata kabisa. Unaposoma qurani 61:9 inapeana ujumbe huo kamili…kwa kunukuu tu inasema;….yeye ndiye aliyemleta mtume wake kwa uongofu, ili kuifanya ishinde dini zote… Kwa hivyo ni dini ndio lakini ya kushindanda tu. Ukisoma hadithi nyingi tu utapata inaunga mkono jambo hili. YESU KRISTO Anatoa tahadhari kwa wale ambao wanamfuata ambaye hajui aendako. Mathayo 15:14… Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili. Mpendwa, maandiko yanasema kuwa ukiwa Mkristo basi utamtukuza MUNGU katika hilo JINA…1 Petro 4:15… Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. 16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo. Kwa hivyo mtukuze MUNGU kwa kuwa wewe ni Mkristo na utazidi kuwa Mkristo wa kweli. BWANA YESU KRISTO Akuongoze na Akubariki sana. Mwalimu Stephen Kasinah 0722 935 429
No comments yet. Be the first to comment!