YESU KRISTO NDIYE ANAFAIDA TUNAPOMFUATA.

12 March 2026

NANI WA FAIDA UKIMFUATA. Hii ni mada nzuri sana ambayo wewe unafaa kuielewa sana. Lakini kwa nini sasa YESU katika hii mada ya utume? Wakolosai 3:11…Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote. Kwa hivyo ni wazi kwamba YESU KRISTO anaingia mahali popote pale. Sasa hii mada lazima tuelewe mambo Fulani. Katika kitabu cha Amosi 3:7… Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Kwa hivyo ni wazi kwamba lazima BWANA MUNGU awafunulie watumishi wake siri yake. Na ndio maana ametufunulia hio siri katika maandiko matakatifu ya Biblia hebu. Hebu soma 1 wakorintho 4:1… Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Kwa hivyo hii inatufunza kwamba sisi tunayo hio siri ya MUNGU. Hio siri ni ipi? Wakolosai 2:2… ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo; kumbe hio siri ni KRISTO. Swali la kujiuliza ni je! Marafiki zetu wanayo siri ya Mungu? Qurani 6:50…inasema kwamba hawana siri ya Mungu. Sasa kwanini tuseme kwamba YESU ndiye mtume wa ulimwengu wote na wala sio Muhammad? Ni kwa sababu Qurani yenyewe inadhibitisha hilo. Qurani 29:27…inaweka sawa mazingira ya kwamba Unabii na kitabu vimetoka katika uzao wa Isaka na Yakobo. Na ndio sababu katika Mwanzo 49:10… Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. 11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu. Kwa hivyo tunapata kwamba ni katika uzao huo tu ndio mtume wa ulimwengu anatokea. Na andiko hilo linatimia tu kwa nani? Yohana 12:12… Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu; 13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli! 14 Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa, 15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda. 16 Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo. Kumbe yote hayo yalikuwa yakimlenga Bwana Yesu kristo. Jambo lingine ni kwamba Yesu mwenyewe alishuhudia hivi, Luka 24:44… Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Swali aliandikiwa vipi? Katika kitabu cha Isaya 42:6…Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; utabiri huo ulitimia? Ndio ulitimia kwa Bwana Yesu Kristo katika Yohana 8:12… Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. Kwa hivyo unaona maandiko yanatimia tu kwa Bwana Yesu. Pia tusome tu kwa huyo huyo Isaya 49:6… naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia. Kumbe Yesu atakuwa mtawala mpaka miishao ya dunia sio Israeli tu. Kipengele kingine ni hiki, YESU KRISTO hakufanya dhambi wala hila haikuonekana kinywani mwake, utapata hayo katika kitabu cha 1 Petro 2:22 na pia mwenyewe anajishuhudia kwamba hana dhambi, Yohana 8:46…Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki? Lakini Muhammad yeye anazo dhambi. Soma Qurani 48:2…ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yanayokuja…pia soma Qurani 47:19…jua ya kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na (dhambi) za waislamu wanaume na waislamu wanawake. Na mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi na mahali penu pa kukaa. Swali la kujiuliza hapo ma hali waislamu watakaa ni wapi? Qurani 19:71…wala hakuna yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia hio (jehanamu). Ni wajibu wa Mola wako uliokwishahukumiwa. Kumbe wanaomfuata Muhammad kwama mtume wa ulimwengu hatima yao ni moto wa jehanamu na ndio akasema kwamba hajui atakavyofanywa wala watakavyofanywa waislamu wanaomfuata, Qurani 46:9. Lakini ukimfuata Bwana Yesu Kristo hatima yako itakuwa vipi? Yohana 14:1… Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Kumbe tukimfuata Bwana Yesu tutakuwa salama. Kwanini bado tunamkataa Muhammad? Ni kwa sababu ya hii, Qurani 80:1…Alikunja (mtume) paji na akageuza uso 2. kwa sababu alimjia kipofu. Muhammad kipofu alimjia na hakutaka kumhudumia. Sasa huyu hawezi akawa mtume wa ulimwengu kwa sababu kitendo hicho Mungu Alimkasirikia. Lakini Bwana Yesu Kristo aliwamfanyia kipofu nini? Marko 10:46… Wakafika Yeriko; hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia. 47 Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. 48 Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu. 49 Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita. 50 Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. 51 Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. 52 Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani. Ona vile Yesu alivyomfanyia yule kipofu alimuhudumia na yule kipofu akamfuata Bwana Yesu Kristo. Yeye Muhammad alipingana na Mungu hadi Mungu akalalamika sana soma Qurani 66:1. Sasa marafiki zetu waislamu wanasoma hili fungu na kudai kwamba Mungu aliwaahidi waisraeli na hangeweza kutangua ahadi yake kwa waisraeli. Fungu lenyewe hili hapa, Matendo 13:23…Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi; ni kweli Mungu aliahidi kabisa halipingiki. Aliahidi wapi? Mika 5:2…Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele. Huu unabii ulitimia wapi? Katika Mathayo 2:6… Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli. Kwa hivyo ulitimia kwa Bwana Yesu na ndio sababu akasema hivi katika Mathayo 15:24…Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Kwanini aliyasema hayo? Marko 7: 27… Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa. Kumbuka hatuoni mahali popote Yesu alimwita yule mwanamke mbwa, soma hapo hapo Mathayo 15:28… Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile. Kwa hivyo alikuwa aanze Israeli kwanza kisha ulimwengu mzima kama vile Mika anavyomalizia katika aya ya 4. Mika 5:4…Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za Bwana, kwa enzi ya jina la Bwana, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia. Yohana naye anasema hivi, Yohana 1:29…Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Lakini wanaosema Muhammad ni mtume ni akina nani? Qurani 63:1…wanafiki ndio wanasema Muhammad ni mtume wa Mungu na eti Mungu anashuhudia kwamba yeye ni mtume wake…lakini kauli ya Mungu anasema, hakika wanafiki ni waongo wanasema wasiyoyajua. Sasa tuzingatie aya ya 5 inasema hivi…Na wanapoambiwa: njooni ili mtume wa Mwenyezi Mungu akuombeeni msamaha (kwa makosa yenu mliyoyafanya),’’huvigeuza vichwa vyao ( kwa kuonyesha kuwa hawataki) na unawaona wanajizuia na wakijiona wakubwa. Sasa jiulize ni nani anayesamehe dhambi maana Muhammad hawezi akasamehe dhambi kwa kuwa ana dhambi Soma Qurani 48:2. Lakini huyu mtume atakaye wasamehe dhambi ama anayesamehe dhambi? 1 Yohana 2:1… Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, 2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. Kumbuka Yohana anazungumza kama Muisraeli na ndiye anasema Yesu ndiye wa ulimwengu wote. Kama Muhammad ni mtume, basi hapa ndipo alitumwa Qurani 26:214…na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe. Hapo tu ndipo alitumwa kama yeye ni mtume. Swali la kujiuliza ni nani alimpa utume huyu Muhammad maan ukisoma Qurani 4:79 inaonyesha kwamba kuna hawa “nasi” ambao walimfanya Muhammad kuwa mtume Mungu akiwa shahidi. Waislamu wangetusaidia hawa ni akina nani? Na pia watupe andiko Mungu anasema amemtuma Muhammad kuwa mtume wake. Hio ni kuonyesha kwamba YESU KRISTO ndiye mtume wa ulimwengu wote na hilo halipingiki. Ubarikiwe sana na MUNGU akuzidishie sana kuelewa Zaidi maneno yake na udumu katika pendo lake. MUNGU AWE NAWE DAIMA MILELE AMINA. End time Loudcry tv 0722935429 0

Comments (0)

No comments yet. Be the first to comment!

← Back to Blog